// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MANGALA SASA NDIYE BEKI GHALI ENGLAND - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MANGALA SASA NDIYE BEKI GHALI ENGLAND - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, August 12, 2014

    MANGALA SASA NDIYE BEKI GHALI ENGLAND

    KLABU ya Manchester City imemfanya Eliaquim Mangala kuwa beki ghali zaidi kwa sasa katika historia ya soka ya Uingereza, baada ya kumnunua kwa Pauni Milioni 31.9 beki huyo wa akti wa Ufaransa kutoka FC Porto.
    Ndoto za Mangala kuhamia Ligi Kuu ya England hatimaye zilitimia jana baada ya kuupiku uhamisho wa Pauni Milioni 30 uliomtoa Rio Ferdinand Leeds kuhamia Manchester United mwaka 2002.
    Mangala, mwenye umri wa miaka 23, anakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na City baada ya kukubali Mkataba wa miaka mitano na kocha Manuel Pellegrini anaamini huyo ni moja ya mabeki wa thamani ya juu Ulaya na atadhihirisha thamani yake uwanjani.

    Beki ghali: Eliaquim Mangala amesaini Manchester City kutoka Porto kwa Pauni Milioni 32

    MABEKI GHALI LIGI KUU ENGLAND 

    Eliaquim Mangala - Pauni Milioni 32- kutoka Porto kwenda Man City, Agosti 2014
    Rio Ferdinand - Pauni Milioni 30 kutoka Leeds kwenda Man Utd, Julia 2002
    Luke Shaw - Pauni Milioni 27 kutoka Southampton kwenda Man Utd, Juni 2014
    Joleon Lescott - Pauni Milioni 22 kutoka Everton kwenda Man City, Agosti 2009
    David Luiz - Pauni Milioni 21 kutoka Benfica kwenda Chelsea, Januari 2011
    Mfaransa huyo baada ya kukamilisha uhamisho wake amesema; "Mimi ni aina ya mchezaji ambaye naingia uwanjani kushinda,".
    "Siachi kitu chochote, wakati wote napambana hadi mwisho na nina matumaini kwa desturi yangu huu, tutashinda mataji mengi msimu huu.
    "Nina furaha sasa kwa sababu nitakuwa tayari kuanza maisha mapya. Nitakuwa tayari kufanya mazoezi tena. Ilikuwa vizuri kwenda mapumziko, lakini baada ya muda unarudi kazini.
    "Ninakwenda kukimbia kila siku na kufanya mazoezi kwenye gym. Mapumziko ni mazuri, lakini yakiwa marefu, inakuwia vigumu kurudi vizuri. Nafikiri nitahitaji muda, ila nitapambana kurudi katika ubora wangu kwa asilimia 100 haraka iwezekanavyo.
    "City ni klabu kubwa Ulaya. Kwangu, ilikuwa hatua muhimu kuondoka Porto na kujiunga na Manchester City ili kusonga mbele kimafanikio. Nataka kushinda mataji na ninaamini nitafanya hivyo,"amesema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MANGALA SASA NDIYE BEKI GHALI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top