KLABU ya West Ham imeimarisha safu yake ya ushambuliaji kwa kumsajili Diafra Sakho kutoka FC Metz ya Ufaransa.
The Hammers imetangaza katika tovuti yake kwamba mpachika mabao huyo mwenye umri wa miaka 24 amesaini mkataba wa miaka minne, ingawa dau halikutajwa.
Mchezaji huyo wa Senegal anahamia England baada ya kung'ara Metz, akifunga mabao 43 katika misimu miwili iliyopita na kuiwezesha klabu hiyo kurejea Ligi Kuu.



.png)
0 comments:
Post a Comment