KLABU ya Manchester City imewekeza jumla ya Pauni Milioni 175 kikosini make ndani ya siku nne, kufuatia mshambuliaji Sergio Aguero kuaini Mkataba mpya wa miaka mitano na mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England Alhamisi usiku.
Mshahara mpya wa Aguero wa Pauni 150,000 kwa wiki umethibitishwa baada ya kusainishwa pia mikataba mipya kwa kiungo David Silva na beki Vincent Kompany ambao watadumu Etihad hadi mwaka 2019. City iliianza wiki kwa kutoa Pauni Milioni 32 kumsajili beki wa FC Porto, Eliaquim Mangala anayeweka rekodi ya beki ghali katika historia ya soka ya Uingereza.
0 comments:
Post a Comment