KOCHA Louis van Gaal ameendelea kuwapa raja mashabiki wa Old Trafford baada ya Manchester United leo kuifunga Valencia mabao 2-1 katika mchezo wa kirafiki.
Sifa zimuendee Marouane Fellaini aliyefunga bao la ushindi dakika ya 90 na ushei katika mchezo ambao, Wayne Rooney alikosa penalti kipindi cha kwanza iliyookolewa na Diego Alves.
United ilitangulia kupata bao kupitia kwa Darren Fletcher dakika ya 49 kabla ya Rodrigo kuisawazishia Valencia dakika ya 71.
Kikosi cha Manchester United: De Gea; Jones, Smalling, Blackett; Young, Fletcher, Herrera, James; Mata; Rooney, Hernandez
Valencia: Alves; Barragan, Vezo, Otamendi, Gaya; Parejo, J. Fuego, Andre Gomes; Feghouli, Alcacer, Rodrigo



.png)
0 comments:
Post a Comment