MSHAMBULIAJI Luis Suarez amepunguziwa adhabu ya kufungiwa miezi mine kujishughulisha na soka kwa kumng'ata Giorgio Chiellini wa Italia, Mahakama ya Usuluhishi ya Mchezo (CAS) imeamua leo mjini Lausanne.
![]() |
| Ahueni; Suarez akiwa amezungukwa na Waandishi wa Habari leo nje ya CAS |
Uamuzi huo unamaanisha Suarez atakuwa tayari kuichezea kwa mara ya kwanza Barcelona Jumatatu katika mchezo wa kirafiki wa kuwania taji la Joan Gamper dhidi ya timu ya Liga MX, Leon Uwanja wa Nou Camp kama atakuwa fiti kaisi cha kutosha.
Mpachika mabao huyo wa Uruguay alifungiwa kujihusisha na shughuli zote za soka Julai 1 mwaka huu baada ya tukio hilo katika mchezo wa makundi Kombe la Dunia dhidi ya Italia Juni 24 mjini Natal.
Suarez alifungiwa baaada ya kumng'ata Giorgio Chiellini (kushoto)
Na sasa adhabu yake imepunguzwa badala ya kutojihusisha kabisa na masuala ya soka, Suarez ataruhusiwa kutambulishwa Barca, kufanya mazoezi, kuiangalia timu yake ikicheza na kushiriki shughuli zote za promosheni za timu.
CAS imesema adhabu ya FIFA dhidi ya Suarez ilikuwa jail mno kwa mchezaji huyo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 atashiriki mazoezi ya mara mbili kwa siku ya timu yake, Barcelona kuanzia leo Saa 3.30 asubuhi na 12.30 jioni kwa saa za Hispania.
Suarez hataruhusiwa kuichezea Barcelona hadi Oktoba 26, wababe hao wa Katalunya watakapomenyana na Real Madrid katika La Liga Uwanja wa Bernabeu, na ataendelea kukosa mechi nane za Uruguay za mashindano.
Pamoja na hayo, Mahakama hiyo imeondoa kipengele cha kumzuia kabisa kujishughulisha na masuala ya soka.
Taarifa ya Mahakama imesema: "Kusimamishwa kwa miezi mine kutahusu mechi za mashindano pekee na si tena kutojihusisha na masuala ya soka kabisa (kama kufanya mazoezi, matukio ya promosheni na mambo ya utawala).'
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool alihamishiwa Barcelona kwa dau la Pauni Milioni 75 baada ya kufungiwa, lakini hakuwahi kutambulishwa katika klabu yake mpya kutokana na adhabu yake hiyo.



.png)
0 comments:
Post a Comment