KLABU ya Southampton imekamilisha usajili wa kipa wa England, Fraser Forster kwa dau la Pauni Milioni 10 kitoka mabingwa wa Scotland, Celtic.
Kocha wa Watakatifu, Ronald Koeman amesema jana baada ya kipigo cha 1-0 katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na msimu kutoka kwa Bayer Leverkusen kwamba dili ni kama limetimia baada ya klabu hizo kukubaliana ada ya uhamisho na mchezaji tayari amefanyiwa vipimo.
Na Jumamosi jioni klabu hiyo ilitoa taarifa kwenhye tovuti yake ikithibitisha usajili wa mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 26.
0 comments:
Post a Comment