• HABARI MPYA

    Saturday, August 16, 2014

    LIVERPOOL YASAJILI BONGE LA BEKI LA HISPANIA

    BEKI wa pembeni wa Hispania, Alberto Moreno amesaini Liverpool kwa ada ya Pauni Milioni 12.
    Makubaliano ya uhamisho huo yalifikiwa mapema wiki hii, lakini ikachukua muda hadi sasa klabu hiyo inamtambulisha rasmi mchezaji huyo. 
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa akifanya vizuri kwa miaka miwili iliyopita - ikiwa ni pamoja na kuwamo kwenye kikosi cha U21 cha Hispania kiloichochukua ubingwa wa Ulaya mwaka 2013, na kung'ara Sevilla.
    Moreno alishinda taji la Europa League na Sevilla msimu uliopita na alimwaga machozi baada ya kufungwa na Real Madrid katika mechi ya UEFA Super Jumanne.

    Kijana mpya: Liverpool imemtangaza rasmi Alberton Moreno leo
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIVERPOOL YASAJILI BONGE LA BEKI LA HISPANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top