TUKIO la ghafla zaidi na la kushitua katika anga ya soka Tanzania lilikuwa ni kufukuzwa kwa aliyekuwa kocha wa Simba SC, Zdravko Logarusic raia wa Croatia.
Siku moja baada Wekundu wa Msimbazi kufungwa mabao 3-0 na ZESCO United ya Zambia katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Loga alifukuzwa.
Rais wa Simba SC, Evans Aveva alisema Loga amefukuzwa baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji baada ya kuona anakiuka maadili ya klabu.
Aveva alijitetea kwa kusema uamuzi huo umekuja baada ya kujaribu mara kadhaa kumuonya mwalimu huyo na kuona anashindwa kubadilika.
Sasa kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2009/2010, Patrick Phiri anarejea Dar es Salaam kuifundisha klabu yake ya zamani, Simba SC.
Mzaliwa huyo wa Mei 3 mwaka 1956, alifanya kazi kwa awamu tatu tofauti akiwa na Wekundu hao wa Msimbazi kati ya mwaka 2004 na 2010 na kwa mafanikio makubwa- na sasa anataka kurejesha enzi.
Mzambia huyo alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu akiwa na Simba SC, misimu ya 2004/2005 na 2009/2010 na pia alishinda Makombe ya Tusker mwaka 2005 la Tanzania na Kenya.
Phiri ni kocha anayekubalika zaidi mbele ya mashabiki wa Simba SC miongoni mwa makocha waliowahi kufundisha klabu hiyo- rekodi yake ya kukumbukwa zaidi ikiwa ni kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2009/2010 bila kufungwa hata mechi moja.
Lakini pia, namna alivyoweza kuiongoza Simba SC kuwatambia watani wa jadi, Yanga SC ni jambo lingine linalomfanya awe kocha mwenye heshima ya kipekee Msimbazi.
Katika awamu zote tatu alizofundisha Simba SC awali, Phiri hajawahi kufukuzwa- kwani amekuwa akiondoka mwenyewe kwa sababu mbalimbali.
Kwa sasa, mume huyo wa Cecilia Mutale waliyezaa naye watoto wawili, Melesianiah na Patrick Junior, anarejea Simba SC akitokea Green Buffaloes ya Ligi Kuu ya Zambia.
Phiri ni kocha mwenye mafanikio tangu anacheza soka katika klabu za Rokana United (sasa Nkana F.C.) na Red Arrows zote za nyumbani kwao, Zambia kama mshambuliaji.
Alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Zambia kilichocheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 1978 na 1982, kabla ya kuiwezesha Chipolopolo kufuzu kwa AFCON ya mwaka 2008 nchini Ghana.
Akiwa kocha, Phiri pia aliiongoza timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Zambia kucheza Fainali za kwanza kabisa za Kombe la Dunia nchini Nigeria mwaka 1997 kabla ya kushinda tuzo ya kocha bora wa mwaka nchini mwake mwaka 1999.
Loga ambaye aliongezewa Mkataba wa mwaka mmoja mwezi uliopita- ameondoka Simba SC baada ya kuiongoza katika mechi 21 tangu Desemba mwaka jana, kati ya hizo akishinda nane, sare tano na kufungwa nane.
Loga aliyerithi mikoba ya Mzalendo, Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’, aliikuta Simba SC bado ipo kwenye mbio za ubingwa msimu uliopita, lakini mwishowe ikamaliza nafasi ya nne nyuma ya Mbeya City, Yanga SC na Azam FC mabingwa.
Baada ya kumaliza msimu, Loga alitayarisha ripoti yake juu ya wachezaji wa kuachwa na aina ya wachezaji ambao anataka wasajiliwe.
Loga alikwenda likizo nyumbani kwao, akiachia uongozi ufanyie kazi mapendekezo yake ya kitaalamu na aliporejea, akasaini Mkataba mpya.
Loga aliajiriwa Simba SC chini ya uongozi uliomaliza muda wake, wa Alhaj Ismail Aden Rage na alimaliza mkataba wake wa awali wa miezi sita sambamba na ukomo wa uongozi uliopita madarakani.
Katika mwezi wake wa kwanza madarakani, uongozi wa Aveva moja ya mambo ya awali kufanya ni kumuongezea Mkataba Loga.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari, Aveva anasema wamemfukuza Loga kwa sababu hulka na mwenendo wake upo tofauti na desturi na utamaduni wa klabu na wamekuwa wakimuambia mara kadhaa, lakini habadiliki.
Aveva aliingia madarakani Juni 29 na akaanza kazi mapema Julai, wakati Loga alirejea kutoka likizo katikati ya mwezi huo na Agosti 10 kocha anafukuzwa.
Najaribu kuitafuta mara kadhaa ya ambayo uongozi wa Aveva umekuwa ukizungumza na kuwekana sawa na Loga juu ya hulka na mwenendo wake ndani ya kipindi hiki- siioni.
Na kwa kuwa uamuzi ulikuja siku moja tu baada ya Simba SC kufungwa na ZESCO, nazidi kupata wasiwasi juu ya uamuzi huu, kama ulikuwa una sababu za msingi ndani yake, au hasira za kufungwa.
Busara inatufundisha kutoamua wakati tuna hasira, kwa sababu maamuzi mengi ya aina hiyo hufuatiwa na majuto baadaye.
Kweli, rekodi ya Loga haivutii sana tangu ajiunge na Simba SC, lakini kwa kuwa aliaminiwa na kupewa mkataba mpya na timu ikafanya usajili kwa ushauri wake, ina maana alistahili kupewa nafasi nyingine.
Sasa, Loga anaondoka baada ya kutengeneza aina ya Simba aliyoitaka, alielekeza wachezaji wa kusajiliwa na wengine alikuwa anawajua yeye tu, mfano Paul Kiongera.
Phiri anakuja kukuta timu ambayo ilitayarishwa kwa matakwa ya mwalimu mwingine- hivi ikifanya vibaya na akasema tatizo wachezaji kuna wa kupingana naye kweli?
Naamini Simba SC walikuwa wapo katika nafasi nzuri ya kuuthibitisha uwezo wa Loga, baada ya kupewa fursa ya kujenga aina ya timu anayoitaka, tofauti na ile aliyoikuta Desemba mwaka jana.
Lakini pamoja na yote, bado huwezi kuona wapi uongozi wa Aveva ulijaribu mara kadhaa kuzungumza na Loga ili kuwekana sawa, ikiwa waliigia madarakani Juni 29, wakaanza kazi mapema Julai, Loga akarejea kutoka likizo katikati ya mwezi huo na wiki mbili baadaye akapewa Mkataba mpya. Yetu macho, alamsiki.

0 comments:
Post a Comment