• HABARI MPYA

  Monday, January 27, 2014

  MAN UNITED SASA YAGOMBEA BONGE LA BEKI NA CHELSEA

  KLABU ya Manchester United inataka kumsajili beki wa St Etienne, Kurt Zouma lakini inaaminika kinda huyo wa umri wa miaka 19 anaweza kutua Chelsea. 
  Chipukizi huyo alisema mapema mwezi huu kwamba kocha Jose Mourinho alizugumza naye binafsi kwa simu juu ya kuhamia London na klabu hiyo ya Stamford Bridge iko tayari kutoa Pauni Milioni 12.
  United wanafikiri Chelsea imesitisha nia ya kumchukua, lakini habari za ndani zinasema wametoa ofa ya kumsaini kwa mkataba wa miaka mitano Zouma ambaye ni beki wa kati.
  Anatakiwa: Beki wa St Etienne, Kurt Zouma (kushoto) anaweza kutua Chelsea
  Forward planning: Jose Mourinho is aiming to sign young, talented players for his second Chelsea revolution
  Mzee wa mipango: Jose Mourinho anataka kusajili kinda mwenye kipaji Chelsea, Zouma.

  Zouma, ambaye alikuwa anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi 10 kwa kumvunja mchezaji mwenzake mguu, alitarajiwa kuichezeawa timu yake dhidi ya Bordeaux jana, lakini hakucheza baada ya kulalamika anaumwa, kiasi cha kushindwa kufanya mazoezi Alhamisi na ijumaa.
  Big future: Zouma, pictured here in action against Bordeaux, is one of the most coveted young defenders in Europe
  Tishio: Zouma katika mechi dhidi ya Bordeaux, huyu ni mmoja wa mabeki wanaotarajiwa kuwa hodari na kutamba Ulaya
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED SASA YAGOMBEA BONGE LA BEKI NA CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top