• HABARI MPYA

  Friday, January 31, 2014

  KIM KALLSTROM AFAULU VIPIMO VYA AFYA ARSENAL, KLOSE NA QUAGLIARELLA NAO WAPO KWENYE RADA ZA WENGER

  KIUNGO Kim Kallstrom amefaulu vipimo vya afya Arsenal kuelekea kusajiliwa katika siku ya mwisho ya kufungwa pazia la usajili wa dirisha dogo- na pia Washika Bunduki wa London wanaweza kumnasa Miroslav Klose.
  Mchezaji mwenye umri wa miaka wa Spartak Moscow anakaribia kabisa kukamilisha usajili wake The Gunners wakielekea kwenye mechi na Crystal Palace mwishoni mwa wiki hii. 
  Habari hizo zinakuja sambamba na Arsene Wenger kuthibitisha Julian Draxler hatahamia Kaskazini mwa London mwezi huu.
  Wenger pia anakimbizana kuipata saini ya mshambuliaji mkongwe wa Ujerumani, Miroslav Klose kwa Mkataba wa muda mfupi kutoka Lazio na mshambuliaji wa Juventus, Fabio Quagliarella, mwenye umri wa miaka 31, pia yuko kwenye mawindo yake.
  Kimeeleweka: The Gunners wako karibu kukamilisha usajili wa mchezaji kutoka Spartak Moscow, Kim Kallstrom
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIM KALLSTROM AFAULU VIPIMO VYA AFYA ARSENAL, KLOSE NA QUAGLIARELLA NAO WAPO KWENYE RADA ZA WENGER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top