• HABARI MPYA

  Thursday, January 30, 2014

  MBIO ZA UBINGWA ZANOGA ENGLAND, MAN CITY YAKAA KILELENI LAKINI ARSENAL, CHELSEA HAZIKO MBALI NAO

  USHINDI wa mabao 5-0 wa Manchester City dhidi ya Tottenham Hotspur jana katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana, umezidi kunogesha mbio za ubingwa wa ligi hiyo, Arsenal sasa ikishuka hadi nafasi ya pili.
  Mabao ya City jana Uwanja wa White Hart Lane yalifungwa na Sergio Aguero dakika ya 15, Yaya Toure kwa penalti dakika ya 50, Edin Dzeko dakika ya 53, Jovetic dakika ya 78 na Kompany dakika ya 89. 
  City sasa inatimiza pointi 53 baada ya kucheza mechi 23, ikiizidi Arsenal pointi moja na Chelsea pointi tatu. Chelsea jana ililazimishwa sare ya bila kufungana na West Ham United.
  Mwana wa Dhahabu: Sergio Aguero akishangilia baada ya kuifungia bao la kwanza Manchester City Uwanja wa White Hart Lane
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBIO ZA UBINGWA ZANOGA ENGLAND, MAN CITY YAKAA KILELENI LAKINI ARSENAL, CHELSEA HAZIKO MBALI NAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top