• HABARI MPYA

  Jumamosi, Januari 25, 2014

  MBEYA CITY YAZIDI KULA SAHANI MOJA NA YANGA NA AZAM KILELENI

  Na Princess Asia, Bukoba
  MBEYA City imezidi kula sahani moja na Yanga SC na Azam FC kileleni, kufuatia ushindi wa 1-0 leo ugenini dhidi ya wenyeji Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba, Bukoba katika mchezo wa kwanza wa duru la pili Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Shukrani kwake Swita Julius aliyefunga bao hilo pekee kwenye mchezo huo na sasa Mbeya City inatimiza pointi 30 sawa na Azam FC inayokaa nafasi ya pili tu kwa sababu ya wastani mzuri wa mabao, wakati Yanga ipo kileleni kwa pointi zake 31.
  Mbeya City bado inakula sahani moja na Yanga na Azam

  Katika mechi nyingine za ligi hiyo leo, Coastal Union imelazimishwa sare ya 1-1 na JKT Oljoro Uwanja wa Mkwakwani Tanga. Bao la Coastal limefungwa na Yayo Lutimba dakika ya nane, wakati la Oljoro limefungwa na Hamisi Saleh dakika ya 87.
  Yanga imeifunga Ashanti United 2-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mabao yake yakifungwa na Mrundi Didier Kavumbangu na mzalendo David Luhende,bao la wapinzani wao likifungwa na Mnigeria, Bright Obinna, wakati bao pekee la mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Kipre Tchetche limeipa Azam ushindi wa 1-0 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YAZIDI KULA SAHANI MOJA NA YANGA NA AZAM KILELENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top