• HABARI MPYA

  Jumatano, Januari 29, 2014

  ‘KOCHA GUNDU’ AISHUSHA YANGA KILELENI, TANGU AMEKUJA MECHI NNE TIMU IMESHINDA MCHEZO MMOJA TU TENA KWA TAABU

  Na Prince Akbar, Tanga
  MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC wameshushwa kileleni mwa ligi hiyo leo kufuatia kulazimishwa sare ya bila kufungana na Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. 
  Matokeo hayo yanaifanya Yanga itimize pointi 32 baada ya kucheza mechi 15 na kuipisha Azam FC kileleni, ambayo imetimiza pointi 33 baada ya kuifunga Rhino Rangers bao 1-0 leo.  
  Mchezo ulisimama mara mbili kwa dakika moja na ushei ili kupisha zoezi la uokotaji wa chupa za maji zilizojazwa mikojo na tupu zilizorushwa uwanjani na mashabiki wa timu hizo.
  Ubingwa itawezekana? Hans van der Pluijm ameishusha kileleni Yanga SC baada ya mechi mbili tu za Ligi Kuu

  Kwanza ilikuwa dakika ya 29, mashabiki wa Yanga waliporusha chupa baada ya kukerwa na kitendo cha mshika kibendera nambari moja kumezea kitendo cha beki wa Coastal Union Juma Nyosso kuunawa mpira uliopigwa na Didier Kavumbangu katika eneo la hatari.   
  Dakika tisa baadaye, mashabiki wa Coastal nao walirusha chupa langoni mwa Yanga kufutia timu yao kushambuliwa na Wana Jangwani. 
  Yanga SC ilitawala mchezo kipindi cha kwanza na Coastal walitawala kipindi cha pili.
  Huo unakuwa mchezo wa nne Yanga SC kucheza chini ya kocha wake mpya, Mholanzi Hans van der Pluijm ikishinda mechi mmoja tu.
  Awali Mholanzi huyo aliyefukuzwa fukuzwa timu kibao Ghana na St George ya Ethiopia kwa matokeo mabaya kabla ya kutua Jangwani, alitoa sare mbili katika ziara ya Uturuki na akashinda dhidi ya Ashanti United kwa taabu 2-1 Jumamosi katika Ligi Kuu.
  Katika mchezo wa leo uliotawaliwa na vurugu za mashabiki, kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Frank Domayo, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Didier Kavumbangu, Mrisho Ngassa/Nizar Khalfan dk83 na David Luhende/Jerry Tegete dk66.
  Coastal Union; Shaaban Kado, Hamad Juma, Abdi Banda, Juma Nyosso, Mbwana Bakari, Jerry Santo, David Lyanga, Crispian Odula, Lutimba Yayo/Mohammed Miraj dk88, Haruna Moshi na Kenneth Masumbuko/Mohamed Soud dk78.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ‘KOCHA GUNDU’ AISHUSHA YANGA KILELENI, TANGU AMEKUJA MECHI NNE TIMU IMESHINDA MCHEZO MMOJA TU TENA KWA TAABU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top