• HABARI MPYA

  Jumamosi, Januari 25, 2014

  YANGA SC YAANZA NA MOTO LALA SALAMA LIGI KUU BARA, YAICHAPA ASHANTI 2-1, YAKAA SAWA KILELENI

  Na Zaituni Kibwana, Dar es Salaam
  YANGA SC imeuanza vyema mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa ushindi wa tabu wa mabao 2-1 dhidi ya Ashanti United, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Matokeo hayo yanaifanya Yanga SC iendelee kuongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 31 baada ya kucheza mechi 14, wakifuatiwa na Azam FC wenye pointi 30. 

  Hadi mapumziko, hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake, ingawa kosakosa zilikuwa za pande zote mbili.
  Iliwachukua dakika sita tangu kuanza kipindi cha pili Yanga kupata bao la kuongoza, lililotiwa kimiani na Mrundi Didier Kavumbangu dakika ya 51, baada ya kupata pasi nzuri ya Simon Msuva, kufuatia kazi nzuri ya Haruna Niyonzima.
  Hata hivyo, Mnigeria Bright Obinna aliisawazishia Ashanti dakika ya 60 akimalizia pasi ya Hussein Swedi.  
  Yanga ilipata bao lake la ushindi dakika ya 79, baada ya David Luhende kufumua shuti kali, ambalo lilimbabatiza kipa wa Ashanti, Daudi Mwasongwe na kudondokea nyavuni.   
  Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Kevin Yondan, Frank Domayo, Mrisho Ngassa,Haruna Niyonzima, Didier Kavumbangu/Hussein Javu dk85, Said Bahanuzi/Simon Msuva dk35 na David Luhende.
  Ashanti United; Daudi Mwasongwe, Hussein Mkongo, Abdul Mtiro, Shaffi Hassan, Tumba Swedi, Mohammed Fakhi, Abdul Manani/Iddi Suleiman dk47, Fakih Hakika, Bright Obinna/Paul Maona dk85, Hussein Swedi na Joseph Mahundi. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC YAANZA NA MOTO LALA SALAMA LIGI KUU BARA, YAICHAPA ASHANTI 2-1, YAKAA SAWA KILELENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top