• HABARI MPYA

    Thursday, January 30, 2014

    MUOSHWA AKIOSHWA...MOURINHO ALAANI VIKALI WEST HAM UNITED KUPAKI BASI JANA, ASEMA WALICHEZA SOKA YA MWAKA 47

    UMAARUFU wa Jose Mourinho na mafaniko aliyoyapata kutwaa mataji matatu ya Ligi Kuu ya Mabingwa Ulaya, vimetokana na mfumo wa uchezaji wa timu anazofundisha, kucheza kwa kujihami zaidi, maarufu kama kupaki basi.
    Lakini huwezi kuamini leo Mourinho anaulaani vikali mfumo huo wa uchezaji, akiuita wa karne ya 19, ingawa yeye ameutumia miaka ya karibuni tu karne hii na kumjengea heshima na umaarufu mkubwa.
    Baada ya kulazimishwa sare ya 0-0 jana na West Ham United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England, kocha huyo wa Chelsea amemkandia kocha wa wapinzani wake, Sam Allardyce kucheza soka ya karne ya 19.
    Usiku wa jana The Hammers ilipiga shuti moja tu langoni mwa Chelsea iliyopiga mashuti 39 kwenye lango la wapinzani wao hao.
    “Hiyo si ligi bora katika dunia ya soka, hii ni soka ya karne ya 19. Mbaya mno.  Ninamaanisha nini kusema soka ya karne ya 19? Inasababisha kuumizana.
    “Kudanganya, lakini sijui kama hiyo ni kauli nzuri. Kipa alipoteza muda, si baada ya dakika 70, bali kuanzia dakika ya kwanza. Mabeki kumi kwenye boksi. Ngome ngumu. 
    “Ni vigumu kucheza mechi ya soka ambayo timu moja tu inataka kucheza. Nilimuambia Big Sam (Allardyce).
    “Wanataka pointi, lakini kwa sababu wanataka pointi, kuja hapa na kutocheza na kufanya kama walivyofanya… inakubalika? Labda ndiyo. Siwezi kuwa mlalamishi sana, kwa sababu kama ningekuwa kwenye mazingira yao, sifahamu, ningefanya kama wao? Labda ningefanya,” alisema Mourinho. 

    Inakera: Mourinho akilalamika kwa refa wa akiba, Mike Jones
    Screamer: The Chelsea boss was frustrated all evening as his side couldn't find a way through West Ham
    Hasira: Kocha wa Chelsea alikasirishwa na mfumo wa uchezaji wa kujihami wa West Ham usiku wa janaOne-way traffic: Our Match Zone shows Chelsea's dominance
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MUOSHWA AKIOSHWA...MOURINHO ALAANI VIKALI WEST HAM UNITED KUPAKI BASI JANA, ASEMA WALICHEZA SOKA YA MWAKA 47 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top