• HABARI MPYA

  Jumamosi, Januari 25, 2014

  KIPRE TCHETCHE AITAKATISHA AZAM CHAMAZI, YANGA HAWANA RAHA KILELENI

  Na Prince Akbar, Chamazi
  BAO pekee la mshambuliaji wa Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche jioni ya leo limeipa ushindi wa 1-0 Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro.   
  Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Isihaka Shirikisho wa Tanga, Tchetche alifunga bao hilo baada ya kupokea pasi nzuri ya Joseph Lubasha Kimwaga na akiwa katikati ya mabeki wa Mtbwa Sugar, akaumiliki mpira vyema na kufumua shuti kali lililotinga nyavuni.
  Asante kwa pande; Kipre Tchetche kulia akipongezana na Joseph Kimwaga aliyempa pasi ya kuifungia Azam bao pekee leo

  Pamoja na kutoka uwanjani wakiwa nyuma kwa 1-0, Mtibwa inayofundishwa na beki wake wa zamani, Mecky Mexime ilicheza vizuri na kutoa upinzani kwa Azam kipindi cha kwanza. 
  Kipindi cha pili, mchezo ulipendeza zaidi, Mtibwa wakisaka bao la kusawazisha na Azam wakilinda na kusaka la kuongeza, lakini mwisho matokeo yalibaki 1-0.
  Azam inaendelea kuwa nyuma ya vinara wa ligi hiyo Yanga SC wenye pointi 31, wakizidiwa pointi moja tu na mabingwa hao watetezi pia.
  Kipre Tchetche akiwashughulisha walinzi wa Mtibwa leo Chamazi 

  Kikosi cha Azam FC leo kilikuwa; Mwadini Ali, Malika Ndeule, Erasto Nyoni, Said Mourad, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Brian Umony/Ismael Kone dk13/Khamis Mcha dk71, Kipre Tchetche na Joseph Kimwaga/Seif Karihe dk69.
  Mtibwa Sugar; Hussein Sharrif, Hassan Ramadhani, Said Mkopi, Salim Mbonde, Salvatory Ntebe, Shaaban Nditi, Shaaban Kisiga, Masoud Ally/Abdallah Juma dk62, Juma Luizio/Mussa Mgosi dk84, Jamal Mnyate na Vincent Barnabas/Mohamed Salum dk75.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KIPRE TCHETCHE AITAKATISHA AZAM CHAMAZI, YANGA HAWANA RAHA KILELENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top