• HABARI MPYA

  Jumatatu, Januari 20, 2014

  KIPRE TCHETCHE AWATANGAZIA VITA TAMBWE NA KIIZA, AWAAMBIA MFUNGAJI BORA NI YEYE TU HAKUNA MWINGINE

  Na Dina Ismail, Dar es Salaam
  MFUNGAJI bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Kipre Herman Tchetche raia wa Ivory Coast  amesema kwamba hana shaka atafanikiwa kutetea tuzo yake ya ufungaji bora msimu huu   
  Mshambuliaji huyo wa Azam FC ya Dar es Salaam, ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba mzunguko wa pili wa Ligi Kuu unaoanza mwishoni mwa wiki utakuwa wakati mzuri kwake kufunga mabao.
  Ni yangu tu hii; Kipre Tchetche kushoto akiwa na ndugu yake, Kipre Balou baa ya kuchukua tuzo yake ya ufungaji bora Ligi Kuu mwaka jana 

  “Mzunguko wa kwanza kwa kweli sikuwa fiti kwa asilimia 100, ila ila kwa sasa niko fiti kabisa na ninaingia vitani kwa ajili ya mambo mawili makubwa. Kwanza kuisaidia Azam kutwaa ubingwa na pili mimi kutwaa ufungaji bora,”alisema.
  Amesema ni kweli kuna ushindani katika mbio za kiatu cha dhahabu msimu huu, lakini atapambana kadiri ya uwezo wake kuhakikisha anawapiku walio juu yake ili atetee kiatu chake.
  Kipre aliyeibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita kwa mabao yake 17, hadi mzunguko wa kwanza msimu huu unamalizika alikuwa amekwishafunga mabao nane.
  Kuelekea mzunguko wa pili wa Ligi Kuu, Mrundi Amisi Tambwe wa Simba SC anaongoza kwa mabao yake 10, akifuatiwa na Tchetche, Hamisi Kiiza wa Yanga SC, Juma Luizio wa Mtibwa Sugar, Elias Maguri wa Ruvu Shooting wenye mabao nane kila mmoja, Themi Felix wa Kagera Sugar mabao saba. Wengine walio kwenye mbio hizo ni Mrisho Ngassa wa Yanga SC mabao sita, Jerry Tegete, Didier Kavumbangu wa Yanga, Tumba Swedi wa Ashanti United na Mwagane Yeya wa Mbeya City ambao kila mmoja ana mabao matano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KIPRE TCHETCHE AWATANGAZIA VITA TAMBWE NA KIIZA, AWAAMBIA MFUNGAJI BORA NI YEYE TU HAKUNA MWINGINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top