• HABARI MPYA

  Jumamosi, Januari 25, 2014

  ESSIEN AHAMIA AC MILAN, CHELSEA ROHO KWATUUUU

  KLABU ya Chelsea imefikia makubaliano ya kumuuza kiungo Michael Essien kwa AC Milan, timu hiyo ya Ligi Kuu ya England imetangaza.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 amejikuta anakosa namba kikosi cha kwanza Stamford Bridge tangu arejee Real Madrid alikokuwa anacheza kwa mkopo msimu uliopita na amepewa ruhusa na kocha Jose Mourinho kuondoka.
  Taarifa ya Chelsea jana usiku imesema kwamba tayari wamefikia makubalkiano na Milan juu ya mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ghana.
  Tabasamu tupu: Michael Essien anajiandaa kusaini AC Milan baada ya miaka tisa ya kuitumikia ChelseaPopular arrival: AC Milan urgently need to strengthen after a disappointing first half of the season
  Mtu maarufu amewasili: Essien akimsainia shabiki wa AC Milan
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ESSIEN AHAMIA AC MILAN, CHELSEA ROHO KWATUUUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top