• HABARI MPYA

  Monday, January 20, 2014

  RIBERY AWAPONDA FIFA KUMPA RONALDO BALLON D'OR, ASEMA AMEDHULUMIWA MCHANA KWEUPE HAKI YAKE

  NYOTA wa Bayern Munich, Franck Ribery ameuponda mfumo wa upigaji kura za kuchagua Mwanasoka Bora wa Dunia wa FIFA, Ballon d'Or na kusema alistahili zaidi kushinda tuzo hiyo kuliko Cristiano Ronaldo, kwa sababu alishinda mataji matano mwaka 2013, wakati mpinzani wake wa Real Madrid hakushinda chochote.
  Mfaransa huyo alikubali kushika nafasi ya tatu nyuma ya mshindi, Ronaldo na Lionel Messi aliyekuwa wa pili katika sherehe za tuzo zilizofanyika mjini Zurich, Uswisi Jumatatu iliyopita na pia amesema tuzo binafsi si muhimu kwake.
  Big names: Cristiano Ronaldo (left), Lionel Messi (centre) and Ribery ahead of the Ballon d'Or award
  Ribery alitwaa mataji ya Bundesliga, Kombe la Ujerumani, Ligi ya Mabingwa, Super Cup ya UEFA na Klabu Bingwa ya Dunia akiwa na Bayern mwaka 2013.Nyota huyo wa Ufaransa pia alisema kwamba yalifanyika mabadiliko katika mfumo wa upigaji kura mwaka huu kumsaidia Ronaldo, kwa kuongeza muda wa kupiga kura wakati nyota huyo wa Ureno alikuwa kwenye mazingira ya kuiwezesha nchi yake kuitoa Sweden katika kinyang'anyiro cha tiketi ya Kombe la Dunia.
  Champion: Ribery believes his medal haul of five trophies in 2013 should have seen him win the Ballon d'Or
  All smiles: Ribery celebrates winning the FIFA Club World Cup after Bayern Munich beat Raja Casablanca
  Hasira zake hazikuishia kwenye tuzo hiyo tu, bali pia uteuzi wa kikosi bora cha wachezaji 11 wa FIFA wa mwaka- kuhusisha wachezaji watatu tu wa Bundesliga, licha ya Fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2013 kuzikutanisha Bayern na Borussia Dortmund.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RIBERY AWAPONDA FIFA KUMPA RONALDO BALLON D'OR, ASEMA AMEDHULUMIWA MCHANA KWEUPE HAKI YAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top