• HABARI MPYA

  Jumatano, Januari 29, 2014

  ARSENAL KWELI 'DISKO TOTO', YALAZIMISHWA SARE 2-2 NA VIBONDE SOUTHAMTPON...SASA MAN CITY NA CHELSEA NJIA NYEUPEE KUELEKEA KWENYE UBINGWA

  BAO la Adam Lallana limeosha kuipa sare ya 2-2 Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya vinara, Arsenal ambao sasa wanawafungulia milango Manchester City na Chelsea kwenye mbio za ubingwa. 
  Nyota huyo wa kimataifa wa England alifunga kiasi cha dakika mbili baada ya Santi Cazorla kuifungia Arsenal dakika ya 52 na kumuachia presha kocha Arsene Wenger katika kampeni za ubingwa. 
  Southampton ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Jose Fonte dakika ya 21, lakini Oliver Giroud akaisawazishia The Gunners dakika ya 48. Arsenal walimaliza mechi wakiwa 10 baada ya Mathieu Flamini kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja. 
  Arsenal sasa inakuwa na pointi 52 baada ya kucheza mechi 23, ikifuatiwa na Manchester City yenye pointi 50 na Chelsea pointi 49, ingawa zote zimecheza mechi 22. 
  La uchungu: Nyota wa Southampton, Adam Lallana, katikati, akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la kusawazisha dhidi ya Arsenal
  Yellow peril: Arsenal midfielder Santi Cazorla, centre, celebrates scoring his side's second against Southampton
  Kiungo wa Arsenal, Santi Cazorla, katikati, akishangilia na wenzake baada ya kufunga bao la pili
  French connection: Arsenal striker Olivier Giroud celebrates scoring the equaliser against Southampton
  Mfaransa hatari: Mshambuliaji wa Arsenal, Olivier Giroud akishangilia baada ya kufunga bao la kusawazisha 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ARSENAL KWELI 'DISKO TOTO', YALAZIMISHWA SARE 2-2 NA VIBONDE SOUTHAMTPON...SASA MAN CITY NA CHELSEA NJIA NYEUPEE KUELEKEA KWENYE UBINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top