• HABARI MPYA

  Saturday, January 25, 2014

  MAN UNITED WATAKA KUIPIGA BAO MOJA BAYA SANA CHELSEA...WAKO NJIANI KUPELEKA FEDHA ZA KUNUNUA BEKI AMBALO THE BLUES WANALITAKA

  KLABU ya Manchester United inataka kutumia Pauni Milioni 23 kumsajili beki wa kushoto wa Southampton, Luke Shaw kufuatia kukamilisha usajili wa Juan Mata, uliogharimu Pauni Milioni 37 kutoka Chelsea.
  Ofa hiyo inatarajiwa kupelekwa siku mbili hizi, United ikijaribu kuipiga bao Chelsea katika kuwania saini ya kinda huyo wa umri wa miaka 18.
  Usajili wa Mata unatarajiwa kuvunja rekodi ya mchezaji ghali kusajiliwa na United, ukipiku usajili wa Pauni Milioni 30.75 zilizotolewa kumsajili Dimitar Berbatov mwaka 2008, lakini David Moyes ana njaa ya wachezaji zaidi kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa Januari 31.
  Kifaa kinagombewa: Luke Shaw anatakiwa na klabu kadhaa kubwa, lakini United wanaweza kuwa wa kwanza kupeleka ofa
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED WATAKA KUIPIGA BAO MOJA BAYA SANA CHELSEA...WAKO NJIANI KUPELEKA FEDHA ZA KUNUNUA BEKI AMBALO THE BLUES WANALITAKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top