• HABARI MPYA

  Wednesday, January 29, 2014

  MBEYA CITY YAPUNGUZWA KASI MLANDIZI

  MBEYA City imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Matokeo hayo yanayoipunguza kasi Mbeya City katika mbio za ubingwa, yanaifanya ibakie nafasi ya tatu kwa pointi zake 31, baada ya kucheza mechi 15.
  Ruvu Shooting walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya nne, mfungaji Jerome Lambele kabla ya Deus Kaseke kuisawazishia Mbeya City dakika ya 14. Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, Kagera Sugar wamelazimishwa sare ya bila kufungana na ndugu zao Mtibwa Sugar.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YAPUNGUZWA KASI MLANDIZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top