• HABARI MPYA

  Jumanne, Januari 28, 2014

  AZAM, MBEYA CITY NA YANGA ZAENDELEA NA VITA YA UBINGWA LIGI KUU

  Na Boniface Wambura, Ilala
  LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara,  itaendelea kesho kwa Coastal Union kuikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
  Kiingilio katika mechi hiyo ni sh. 5,000 na sh. 15,000. Nayo Ruvu Shooting na Mbeya City zitapambana kwenye Uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani kwa viingilio vya sh. 10,000 na sh. 5,000.
  Azam watakuwa Chamazi kesho

  Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kutakuwa na mechi kati ya wenyeji Kagera Sugar na Mtibwa Sugar. Viingilio ni sh. 5,000 na sh. 3,000.
  Azam itaumana na Rhino Rangers katika Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Mbagala. Viingilio ni sh. 10,000 na sh. 3,000.
  Yanga SC ambao ndio mabingwa watetezi, wanaongoza Ligi Kuu kwa pointi zao, 31 wakifuatiwa na Azam Mbeya City zenye 30 kila moja baada ya timu zote kucheza mechi 14.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM, MBEYA CITY NA YANGA ZAENDELEA NA VITA YA UBINGWA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top