• HABARI MPYA

  Jumatatu, Januari 27, 2014

  YANGA YAINGIZA MILIONI 86, SIMBA MILIONI 53 MECHI ZA UFUNGUZI LIGI KUU BARA

  Na Boniface Wambura, Ilala
  MECHI za Ligi Kuu ya Vodacom zilizohusisha timu za Simba na Yanga na kuchezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wikiendi zimeingiza jumla ya sh. 139,850,000.
  Yanga iliyoibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ashanti United pambano lake liliingiza sh. 86,035,000 kutokana na watazamaji 14,261. Mechi ya Simba ambayo ilishinda bao 1-0 dhidi ya Rhino Rangers kutoka Tabora iliingiza sh. 53,815,00 kwa watazamaji 9,629.
  Mgawanyo kwa mechi ya Yanga ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 13,123,983.05, gharama za kuchapa tiketi sh. 2,910,300 wakati kila klabu ilipata sh. 20,650,211.50.
  Kikosi cha Yanga kilichomenyana na Ashanti

  Uwanja sh. 10,500,107.54, gharama za mechi sh. 6,300,064.53, Bodi ya Ligi sh. 6,300,064.53, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,150,032.26 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,450,025.09.
  Mechi ya Simba mgawo ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 8,209,067.80, gharama za kuchapa tiketi sh. 2,910,300 wakati kila klabu ilipata sh. 12,595,211.50.
  Uwanja sh. 6,404,344.83, gharama za mechi sh. 3,842,606.90, Bodi ya Ligi sh. 3,842,606.90, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,921,303.45 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,494,347.13.
  Vilevile tiketi zinapatikana kupitia maduka ya CRDB Fahari Huduma ambayo yapo katika maeneo mbalimbali nchini. Watakaonunua kupitia maduka hayo watapata tiketi na kwenda moja kwa moja uwanjani.
  Wakati huo huo: Mauzo ya tiketi za elektroniki kwa mechi tatu kati ya nne za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zitakazochezwa keshokutwa (Januari 27 mwaka huu) tayari yameanza, hivyo wanatakiwa kununua mapema.
  Mechi hizo ni kati ya Coastal Union na Yanga itakayofanyika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Kagera Sugar na Mtibwa Sugar itakayochezwa Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba na ile ya Azam dhidi ya Rhino Rangers kwenye Uwanja wa Azam Complex.
  Kwa washabiki wa Dar es Salaam watakaokwenda Tanga kushuhudia mechi kati ya Coastal Union na Yanga wanashauriwa kuanza safari wakiwa na tiketi zao mikononi, hasa kwa wale watakaonunua kupitia maduka ya Fahari Huduma.
  Tiketi pia zinaweza kununuliwa kupitia mtandao wa M-Pesa kwa kupiga namba *150*03*02#. Kwa wanaotumia CRDB simbanking wanaingia kawaida kwa *150*03.
  Vilevile tunawakumbusha washabiki kuwa kwa viwanja ambavyo tayari vina mfumo wa tiketi za elektroniki hakuna tiketi zitakazouzwa uwanjani, hivyo wanaokwenda kwenye mechi wanatakiwa kuwa na tiketi zao mikononi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA YAINGIZA MILIONI 86, SIMBA MILIONI 53 MECHI ZA UFUNGUZI LIGI KUU BARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top