• HABARI MPYA

  Ijumaa, Januari 31, 2014

  MALKIA KHADIJA KOPA AAMUA KUANZISHA BENDI YAKE

  Na Sauda Mkalokota, Zanzibar
  MWIMBAJI wa nyimbo za Taarabu Tanzania Khadija Omar Kopa ametanzanga kuanzisha bendi yake itakayoitwa Ogopa Kopa’s Morden Taarab  katikati ya mwaka huu wa 2014.
  Amesema hayo wakati akifanya mahojiano na kipindi cha Naksh Nakshi za Pwani cha Zenj FM  Radio Unguja, amesema Machi mwaka huu atasafiri kwenda China kwa ajili ya kununua vifaa vyote vya bendi hiyo ambayo itakuwa kwa ajili ya familia yake.
  Mpinzani kweli anakuja; Mzee Yussuf anayemiliki kundi la Jahazi Modern Taarab kushoto muda si mrefu atapokea upinzani wa kundi jipya la Khadija Kopa kulia

  Amewataja baadhi ya waimbaji watakaokuwamo mbali na yeye mwenyewe ni Hassan Ally na Khanifa Maulid anayetamba na wimbo wa ‘Makavu live’  wote kutoka Kings Morden Taarab.
  "Zaidi tutaibua vipaji vya wasanii wengine chipukizi ambao mtawajua baadaye,"alisema.
  Mbali na hapo Malkia huyo wa mipasho Afrika na Dunia ametambulisha wimbo wake mpya uitwao ‘Lady With Confidence' uliotungwa na Hassan Ally.
  Huu ni wimbo wa kwanza kwa Khadija Kopa kuuachia katika vyombo vya habari mara baada ya kutoka eda ya kufiwa na aliyekuwa mume wake Marehemu Jafari Ally mwezi Juni mwaka 2013.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MALKIA KHADIJA KOPA AAMUA KUANZISHA BENDI YAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top