• HABARI MPYA

  Friday, January 31, 2014

  WEST HAM UNITED YASAJILI BEKI LA NAPOLI KWA MKOPO

  BEKI wa pembeni kushoto wa Napoli, Pablo Armero amejiunga na West Ham kwa mkopo hadi mwishoni mwa msimu huu, klabu hiyo ya Serie A imesema.
  Beki huyo mwenye umri wa miaka 27 alitua Napoli baada ya kucheza kwa mkopo akitokea Udinese mwaka jana, na ameruhusiwa kuondoka na klabu hiyo ya Italia baada ya kukamilisha usajili wa mchezaji kutoka St Etienne, Faouzi Ghoulam.
  West Ham bado haijathibitisha usajili huo, lakini uhamisho wa mkopo wa Armero hadi mwishoni mwa msimu umetangazwa na Napoli.

  Mazungumzo: West Ham imempata beki wa kushoto wa Napoli, Pablo Armero (kulia).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WEST HAM UNITED YASAJILI BEKI LA NAPOLI KWA MKOPO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top