• HABARI MPYA

  Wednesday, January 29, 2014

  AZAM YAPANDA KILELENI LIGI KUU, YANGA YABANWA MKWAKWANI

  AZAM FC imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kufuatia ushindi wa bao 1-0 jioni hii dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Bao pekee la Azam limefungwa na mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche dakika ya 31 kwa shuti kali baada ya kuukuta mpira uliozuiwa na mabeki wa Rhino, kufuatia shuti la ndugu yake kutoka nchi moja, Ismael Kone.
  Azam sasa inafikisha pointi 33 na kupanda kileleni, ikiiteremsha Yanga iliyolazimishwa sare ya bila kufungana na Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanga leo ambyo sasa inakuwa na pointi 32.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM YAPANDA KILELENI LIGI KUU, YANGA YABANWA MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top