• HABARI MPYA

  Ijumaa, Januari 31, 2014

  MALINZI ATIMIZA SIKU 100 TANGU AACHIWE TFF NA TENGA

  Boniface Wambura, Ilala
  KAMATI mpya ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) chini ya Rais Jamal Malinzi, Februari 4 mwaka huu inatimiza siku 100 tangu iingie madarakani katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 28 mwaka jana.
  Hivyo, Rais Malinzi atazungumza na waandishi wa habari Februari 7 mwaka huu kuelezea utekelezaji wa Ilani yake ya uchaguzi. Muda na mahali utakapofanyika mkutano huo mtaarifiwa baadaye.
  Siku 100 madarakani; Jamal Malinzi kulia siku anatambulishwa kuwa rais mpya wa TFF na aliyekuwa rais wa shirikisho hilo kabla yake, Leodegar Tenga kushoto 

  Wakati huo huo: Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetoa sh. milioni 1.5 kwa kila klabu ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
  Uamuzi wa kuzisaidia timu hizo ulifanywa katika kikao cha TPLB kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam ambapo fedha hizo zitalipwa kupitia kwenye akaunti za klabu husika. Hivyo klabu ambazo hazijawasilisha akaunti zao TPLB zinatakiwa kuwasilisha haraka.
  Klabu za FDL ni African Lyon, Burkina Moro, Friends Rangers, Green Warriors, Kanembwa JKT, Kimondo, Kurugenzi Mafinga, Lipuli, Majimaji, Mkamba Rangers, Mlale JKT na Mwadui.
  Nyingine ni Ndanda, Pamba, Polisi Dar es Salaam, Polisi Dodoma, Polisi Mara, Polisi Morogoro, Polisi Tabora, Stand United, Tessema, Toto Africans, Trans Camp na Villa Squad.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MALINZI ATIMIZA SIKU 100 TANGU AACHIWE TFF NA TENGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top