• HABARI MPYA

  Ijumaa, Januari 31, 2014

  OSVALDO ATUA JUVE AKITOKEA SOUTHAMPTON

  MSHAMBULIAJI wa Southampton, Dani Osvaldo amekamilisha uhamisho wa mkopo kuelekea Juventus pamoja na uwezekano wa kununuliwa moja kwa moja kwa dau la Pauni Milioni 16.5 mwishoni mwa msimu.
  Klabu hiyo ya Italia itailipa Southampton Pauni 330,000 kwa sasa na inaweza kuamua kumnunua moja kwa moja Osvaldo kabla ya Mei 31 kwa Mkataba wa Miaka mitatu.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 aliwasili England kwa dau la rekodi katika klabu hiyo kutoka Roma Pauni Milioni 12.9 mwanzoni mwa msimu, lililopanda hadi Pauni Milioni 14.6.
  Uhamisho wa mkopo: Dani Osvaldo (kulia) akipeana mikono na Rais wa Juventus, Andrea Agnelli
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: OSVALDO ATUA JUVE AKITOKEA SOUTHAMPTON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top