• HABARI MPYA

  Wednesday, January 29, 2014

  MASIKINI ROMELU LUKAKU...AONDOKA UWANJANI BAADA YA DAKIKA 25 TU EVERTON IKIADHIBIWA NA LIVERPOOL

  MBALI na kipigo cha mabao 4-0 kutoka Liverpool usiku huu, Everton ilipata pigo lingine baada ya mshambuliaji wake tegemeo, Romelu Lukaku kutolewa nje kwenye machela katika mechi hiyo ya mahasimu wa Merseyside baada ya kuumia
  Mshambuliaji huyo wa mkopo kutoka Chelsea, aliumia kifundo cha mguu baada ya kuangukiwa na mchezaji mwenzake Gareth Barry akijaribu kumzuia bila mafanikio Steven Gerrard kufunga bao la kwanza.
  Nafasi ya Lukaku ilichukuliwa na Steven Naismith dakika ya 25 tu ya mchezo huo Uwanja wa Anfield. 
  Pigo: Romelu Lukaku alivyoumia hapa baada ya kuangukiwa na Gareth Barry (katikati, kushoto)
  Straight off: The Belgian striker had to be removed on a stretcher as Everton's night went from bad to worse
  Moja kwa moja nje: Mshambuliaji huyo wa Ubelgiji akitolewa nje kwa machela baada ya kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MASIKINI ROMELU LUKAKU...AONDOKA UWANJANI BAADA YA DAKIKA 25 TU EVERTON IKIADHIBIWA NA LIVERPOOL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top