• HABARI MPYA

  Friday, January 31, 2014

  KLABU SITA ZATAKA KUMNG'OA CHICHARITO MAN UNITED

  HUKU akiwa nafasi ya uhakika kwenye kikosi cha kwanza Manchester United, hakuna ajabu klabu sita zinataka kumsajili Javier Hernandez.
  Ingawa wakala wake amesema United haitamruhusu nyota huyo wa Mexico kuondoka. 
  Wakala wake amesema: "Nilikuwa Manchester [mapema wiki hii], nilikutana na Mwenyekiti. Javier anachukuliwa kama miongoni mwa wachezaji muhimu katika klabu. Chicharito hataondoka United hata miezi sita ijayo, lakini hatujui kipi kitatokea baada ya Kombe la Dunia,".
  "Kuna klabu Ujerumani, moja Ufaransa, klabu mbili Hispania na mbili zaidi Italia ambazo zinapigana kupata huduma yake,"alisema.
  Amekaa na amefika haondiki: Lich ya kutakiwa na klabu sita, Manchester United imesema Javier Hernandez anabaki Old Trafford
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KLABU SITA ZATAKA KUMNG'OA CHICHARITO MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top