• HABARI MPYA

  Alhamisi, Januari 23, 2014

  MAN MOYES GUNDU TUPU, YATOLEWA KOMBE LA LIGI NA SUNDERLAND

  MZEE wa gundu, David Moyes ameendelea kuwanyima raha mashabiki wa Manchester United, baada ya usiku huu timu hiyo kutolewa katika Nusu Fainali ya Kombe la Ligi, kwa penalti 2-1 kufuatia sare ya jumla ya 3-3 Uwanja wa Old Trafford, Manchester, England.
  Sunderland ilishinda 2-1 katika mchezo wa kwanza nyumbani na leo ikalala 2-1 baada ya dakika 120. Evans alianza  kuifungia United dakika ya 37 na bao hilo likadumu hadi dakika 90 ndipo zikaongezwa dakika 30 na Bardsley akaisawazishia Sunderland dakika ya 119.
   Javier Hernandez 'Chichari' akaifungia United bao la pili dakika ya 120 na ushei na mchezo ukahamia kwenye matuta. Upande wa Man United Darren Fletcher pekee alifunga penalti, wakati Welbeck, Januaj, Jones na Rafael wote walikosa.
  Waliofunga penalti za Sunderland ni Marcos Alonso na Sung-Yong Ki, wakati  Gardner, Steven Fletcher na Johnson walikosa.

  Gutted: David De Gea holds his head after his howler for Phil Bardsley's equaliser on the ngiht
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN MOYES GUNDU TUPU, YATOLEWA KOMBE LA LIGI NA SUNDERLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top