• HABARI MPYA

  Friday, January 31, 2014

  MIDO LA UKWELI CHUJI ‘MUZUZU’ LAINGIA KAMBINI YANGA TAYARI KUPIGA KAZI DHIDI YA MBEYA CITY JUMAPILI, KIIZA DIEGO NA DILUNGA NAO ‘FULL’

  Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
  MIDO la ukweli, Athumani Iddi Athumani ‘Chuji’ ameingia kambini Yanga SC Bagamoyo mkoani Pwani, kujiunga na wenzake kwa maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Habari njema zaidi ni kwamba, kiungo Hassan Dilunga na mshambuliaji Mganda, Hamisi Friday Kiiza ‘Diego’ waliokuwa majeruhi nao wamepona na wamefanya mazoezi na wenzao leo tayari kwa mchezo wa Jumapili.
  Mido la ukweli; Athumani Iddi Chuji ameingia kambini tayari kwa mechi na Mbeya City

  Chuji alisimamishwa na uongozi baada ya mechi dhidi ya mahasimu, Simba SC ya Nani Mtani Jembe ambayo Yanga walilala 3-1 Desemba 21, mwaka jana kwa tuhuma za utovu wa nidhamu ambazo hazikuwekwa wazi.
  Chuji alikosa ziara ya wiki mbili ya timu hiyo nchini Uturuki wakati mapema mwezi huu akitumikia adhabu, kabla ya mwishoni mwa wiki kusamehewa.
  Ofisa Habari wa Yanga SC, Baraka Kizuguto ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba maandalizi ya mchezo wa Jumapili yanaendelea vizuri na wanatarajia kushinda.
  Yanga SC inashika nafasi ya pili katika Ligi Kuu kwa pointi zake 32, ikizidiwa pointi moja na Azam FC iliyo kileleni, wakati Mbeya City ni wa tatu kwa pointi zao 31.
  Mchezo wa Yanga na Mbeya City ambazo mzunguko wa kwanza zilitoka sare ya 1-1 Mbeya unatarajiwa kuwa mkali, kwa sababu timu itakayofungwa itajipunguzia kasi kwenye mbio za ubingwa.
  Tayari Mbeya City wako Dar es Salaam tangu juzi na kocha wake, Juma Mwambusi ametamba wataifunga Yanga Jumapili Uwanja wa Taifa.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MIDO LA UKWELI CHUJI ‘MUZUZU’ LAINGIA KAMBINI YANGA TAYARI KUPIGA KAZI DHIDI YA MBEYA CITY JUMAPILI, KIIZA DIEGO NA DILUNGA NAO ‘FULL’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top