• HABARI MPYA

  Alhamisi, Januari 23, 2014

  EZEKIEL KAMWAGA KATIBU MPYA SIMBA SC...ASHA MUHAJI OFISA HABARI

  Bosi mpya; Ezekiel Kamwaga Katibu mpya wa Simba SC
  MWENYEKITI wa Simba SC, Alhaj Ismail Rage anatarajiwa kumtaja Ezekiel Kamwaga kuwa Katibu mpya wa klabu hiyo, nafasi iliyoachwa wazi na Evodius Mtawala aliyejiuzulu baada ya kuteuliwa Shirikisho la SOka la SOka Tanzania (TFF).
  Aidha, mbunge huyo wa Tabora Mjini CCM, atamtaja pia Mwandishi mwandamizi wa magazeti ya Bingwa na Dimba, Asha Muhaji kuwa Ofisa Habari mpya wa klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi, nafasi ambayo inaachwa wazi na Kamwaga anayepanda cheo.
  Habari kutoka ndani ya Simba SC, zimesema kwamba Rage atakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari mchana wa leo Dar es Salaam kutaja wateuliwa hao wapya.
  Kipele kimepata mkunaji; Asha Muhaji ni mpenzi wa damu wa Simba ni mwandishi mzoefu nchini, anakuwa Ofisa Habari mpya wa SImba SC
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: EZEKIEL KAMWAGA KATIBU MPYA SIMBA SC...ASHA MUHAJI OFISA HABARI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top