• HABARI MPYA

  Ijumaa, Januari 24, 2014

  CHELSEA YAMPATA MRITHI WA MATA MAPEMAA, NI NYOTA WA MISRI ALIYEWATUNGUA THE BLUES 'NJE NDANI' LIGI YA MABINGWA

  KLABU ya Chelsea imeipiga bao Liverpool katika kuwania saini ya mshambuliaji wa FC Basle, Mohamed Salah baada ya kumnasa kwa dau la Pauni Milioni 11.
  Wekundu wa Anfield walikuwa mbioni kumsajili mshambuliaji huyo wa Misri na mazungumzo yalikuwa katika hatua nzuri hadil Chelsea ilipopiga gia kubwa na kumpokonya tonge mdomoni Brendan Rodgers Jumatano. 
  Huku Juan Mata akiwa njiani kuhamia Manchester United, The Blues inataka kuziba pengo la Mspanyola huyo kupitia Salah, ambaye aliwavutia katika Lifgi ya Mabingwa msimu huu kwa kuwafunga katika mechi zote za makundi likiwemo la ushindi nchini Uswisi.
  Dili imetiki: Chelsea imemsaini nyota wa Basle, Mohamed Salah, ambaye aliwafunga mabao marmbili msimu huu
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHELSEA YAMPATA MRITHI WA MATA MAPEMAA, NI NYOTA WA MISRI ALIYEWATUNGUA THE BLUES 'NJE NDANI' LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top