• HABARI MPYA

  Jumatano, Januari 29, 2014

  KALI YA BABU WA YANGA, ADAI ETI UPEPO WA MKWAKWANI ULIWAFANYA WASHINDWE KUCHEZA VIZURI LEO

  Na Prince Akbar, Tanga
  BAADA ya sare ya bila kufungana na Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga jioni ya leo, kocha Mkuu wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm amesema kwamba upepo mkali kwenye Uwanja huo uliwafanya washindwe kucheza vizuri kipindi cha pili.
  Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya mechi hiyo, kocha huyo wa zamani wa Berekum Chelsea ya Ghana alisema kwamba kipindi cha kwanza walicheza vizuri, lakini wakashindwa kutumia nafasi walizotengeneza.
  Simon Msuva wa Yanga akimtoka Juma Nyosso wa Coastal Union leo Mkwakwani na chini ni kikosi cha Yanga leo Mkwakwani

  “Tulipoteza mechi kipindi cha kwanza tuliposhindwa kupata bao licha ya kutengeneza nafasi nyingi. Kipindi cha pili tulishindwa kucheza mpira mzuri kutokana na upepo mkali,”alisema.
  Kwa upande wake, kocha wa Coastal, Mkenya Yussuf Chippo amesema kwamba sare hiyo ni jambo jema kwake, kwani amepata pointi moja na hajapoteza mechi.
  “Tulichea vizuri kipindi cha pili, lakini bado tuna upungufu wa kutumia nafasi tunazotengeneza. Tutalifanyia kazi suala hilo,”alisema mwalimu huyo wa zamani wa Bandari ya Mombasa, Kenya na timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars.   
  Yanga SC wameshushwa kileleni mwa ligi hiyo leo kufuatia kulazimishwa sare ya bila kufungana na Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. 
  Matokeo hayo yanaifanya Yanga itimize pointi 32 baada ya kucheza mechi 15 na kuipisha Azam FC kileleni, ambayo imetimiza pointi 33 baada ya kuifunga Rhino Rangers bao 1-0 leo.  
  Yanga SC ilitawala mchezo kipindi cha kwanza na Coastal walitawala kipindi cha pili.
  Huo unakuwa mchezo wa nne Yanga SC kucheza chini ya kocha wake mpya, Mholanzi Hans van der Pluijm ikishinda mechi mmoja tu.
  Awali Mholanzi huyo aliyefukuzwa fukuzwa timu kibao Ghana na St George ya Ethiopia kwa matokeo mabaya kabla ya kutua Jangwani, alitoa sare mbili katika ziara ya Uturuki na akashinda dhidi ya Ashanti United kwa taabu 2-1 Jumamosi katika Ligi Kuu.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KALI YA BABU WA YANGA, ADAI ETI UPEPO WA MKWAKWANI ULIWAFANYA WASHINDWE KUCHEZA VIZURI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top