• HABARI MPYA

  Thursday, January 23, 2014

  MESSI AWA BONGE LA MPISHI BARCA IKIITANDIKA 4-1 LEVANTE ILIYOTOKA NAYO SARE JUMAPILI

  TIMU ya Barcelona imemaliza hasira zake za sare ya Jumapili na Levante kwa kuifumua timu hiyo mabao 4-1 usiku huu kwenye Robo Fainali ya kwanza ya Kombe la Mfalme Uwanja wa Ciutat de Valencia.
  Mkali wa mabao wa Barca, Lionel Messi amecheza mechi ya 400 katika timu hiyo Katalunya usiku huu, ambazo ndani yake ameshinda mataji sita ya La Liga na matatu ya Ligi ya Mabingwa.
  Messi alifanya kazi nzuri akitoa mchango kwa mabao yote manne, ikiwemo hat-trick ya Cristian Tello. Wenyeji walitangulia kupata bao lililofungwa na mchezaji wa zamani wa Liverpool, Nabil El Zhar. 
  Juanfran alijibabatiza mpira uliopigwa na Messi na akaudondoshea kwenye nyavu zake mwenyewe kuisawazishia Barca- kabla ya Tello kufunga mara tatu mfululizo kuipa ushindi mtamu timu yake.

  Happy clapper: Lionel Messi applauds fans after making his landmark 400th appearance for FC Barcelona
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MESSI AWA BONGE LA MPISHI BARCA IKIITANDIKA 4-1 LEVANTE ILIYOTOKA NAYO SARE JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top