• HABARI MPYA

  Jumanne, Januari 28, 2014

  WACHEZAJI WASIOPIMA AFYA MARUFUKU LIGI KUU, HAPANA CHEZEA TFF YA MALINZI WEWE!

  Na Boniface Wambura, Ilala
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limesema kwamba kuanzia Machi 1, mwaka huu mchezaji ambaye hatakuwa amefanyiwa vipimo vya afya hataruhusiwa kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.  
  Taarifa ya TFF leo imesema kwamba, watatoa kwa madaktari wa klabu za Ligi Kuu fomu maalumu za vipimo kwa wachezaji na kila mchezaji atatakiwa kufanyiwa vipimo vyote kama ambavyo fomu imeelekeza.
  Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein akiwakagua wachezaji wa Simba katika michuano ya Kombe la Mapinduzi.

  “Hakuna mchezaji atakayeruhusiwa kuendelea kucheza VPL au kuchezea timu za Taifa kama atakuwa hajafanya vipimo hivyo. Machi 1 mwaka huu ndiyo utakuwa mwisho wa kurejesha fomu za vipimo vya wachezaji,”imesema taarifa hiyo ya TFF chini ya rais wake Jamal Emil Malinzi.
  Aidha, Madakatri wote wa timu za Ligi Kuu kupitia klabu zao wanatakiwa kuwasilisha vyeti pamoja na wasifu wao (CV) TFF kufikia Februari 8 mwaka huu.
  TFF imesema wasifu na vyeti hivyo vinatakiwa ili kuwezesha Kamati ya Tiba ya TFF kuandaa mafunzo kwa wataalamu hao wa tiba kwa wachezaji.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WACHEZAJI WASIOPIMA AFYA MARUFUKU LIGI KUU, HAPANA CHEZEA TFF YA MALINZI WEWE! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top