• HABARI MPYA

    Thursday, January 23, 2014

    KOCHA COASTAL ATAMBA; “OMAN IMETUPA VITU ADIMU, SASA WATATUTAMBUA LIGI KUU BARA”

    Na Mahmoud Zubeiry, Muscat
    KOCHA wa Caostal Union ya Tanga, Mkenya Yussuf Chippo amesema kwamba ziara ya Oman ilikuwa nzuri na yenye mafanikio kwao, kwani wameweza kutimzia malengo ambayo yaliwaleta nchini hapa.
    Coastal ilikuwa hapa tangu Januari 9, mwaka huu na inaondoka leo kurejea nchini moja kwa moja itafikia kwenye mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya JKT Oljoro, Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga Jumamosi.
    Tuko tayari; Kocha wa Coastal Union, Yussuf Chippo

    Chipo amesema kwamba wamenufaika na kambi hiyo waliyoweka katika hoteli ya Taj & Apartments mjini Musact na sasa wanarajea nchini wakiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika Ligi Kuu.
    “Malengo yangu ni kuiweka timu katika nafasi nzuri mwishoni mwa msimu wa Ligi, hicho ndicho kitu ninachokitaka na nina matumaini makubwa nitafanikiwa kuitimiza dhamira hiyo,”alisema kocha huyo wa zamani wa Ulinzi Stars, KCB na Bandari za Kenya.
    Chippo aliyewahi pia kuwa kocha wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Kenya na Msaidizi wa Francis Kimanzi katika timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars mwaka juzi, amesema anaamini vijana wamenufaika sana na kambi hiyo.
    Amesema hana majeruhi hata mmoja kikosini na kuelekea mchezo dhidi ya JKT Oljoro ana matumaini ya kushinda.
    Coastal ilikuja na wachezaji 23 hapa Oman, ambao ni makipa Shaaban Kado na Said Lubawa, mabeki Hamad Juma, Juma Nyosso, Marcus Ndeheli, Ayoub Masoud, Yussuf Chuma, Abdi Banda, Othman Tamim na Mbwana Hamisi ‘Kibacha’.
    Viungo ni Ally Nassor, Jerry Santo, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Razack Khalfan, Ayoub Semtawa, Behewa Sembwana, Keneth Masumbuko, Abdallah Othman ‘Ustadh’, Haruna Moshi ‘Boban’ na washambulaji Danny Lyanga, Atupele Green, Yayo Lutimba na Mohamed Miraj.
    Wakiwa nchini Oman, mabingwa hao wa Ligi Kuu 1988, walicheza mechi nne, kushinda mbili dhidi ya Nadi Oman na Musannaa 2-0 kila mchezo, sare moja 0-0 na Seeb na kufungwa moja na Fanja 1-0.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOCHA COASTAL ATAMBA; “OMAN IMETUPA VITU ADIMU, SASA WATATUTAMBUA LIGI KUU BARA” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top