• HABARI MPYA

    Thursday, January 30, 2014

    THIAGO AFUNGA BOONGE LA BAO LA TIK TAK BAYERN IKICHEZA MECHI YA 43 BILA KUFUNGWA BUNDESLIGA

    BAO la tik tak la Thiago dakika za majeruhi limeipa Bayern Munich ushindi wa 2-1 dhidi ya Stuttgart na kuwawezesha The Bavarians kuendeleza wimbi la ushindi na kutulia kileleni mwa Bundesliga kwa pointi 13 zaidi. 
    Mspanyola huyo mwenye umri wa miaka 22 aliiwahi vizuri krosi ya Rafinha na kubinuka tik tak kuitumbukiza nyavuni dakika ya tatu ya muda wa nyongeza. 
    Mchezaji wa Bayern aliyetokea benchi, Claudio Pizarro alifunga kwa kichwa dakika ya 76 akimalizia mpira wa adhabu wa Thiago, hilo likiwa bao la kusawazisha baada ya Vedad Ibisevic kutangulia kuwafungia wapinzani wao dakika ya 29.
    Bayern sasa imetimiza mechi 43 bila kufungwa Bundesliga ikiwa kileleni kwa pointi zake 50 baada ya kucheza mechi 18, mbele ya Bayer 04 Leverkusen yenye pointi 37 baada ya kucheza mechi 18 pia.

    Bao la ushindi: Thiago Alcantara, kulia, akishangilia baada ya kuifungia Bayern bao la ushindi dhidi ya Stuttgart jana
    Unbelievable technique: Thiago scores a scissor kick against Stuttgart to win the match for Bayern
    Maujuzi: Thiago akifunga kwa tik tak
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: THIAGO AFUNGA BOONGE LA BAO LA TIK TAK BAYERN IKICHEZA MECHI YA 43 BILA KUFUNGWA BUNDESLIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top