GWIJI wa soka duniani, Pele hatashiriki droo ya upangaji Ratiba wa Kombe la Dunia Ijumaa, baada ya kukataa fursa hiyo akihofia kuiweka Brazil katika kundi gumu.
Atakuwepo kwenye zoezi hilo lakini amethibitisha hatashiriki.
"Rais Dilma (Rousseff) amependekeza kwamba niiwakilishe Brazil litakapokuja zoezi kuchagua timu za kuweka kwenye makundi, kazi ambayo nimeifanya mara kadhaa," alisema Pele.
"Nimeamua kukataa ofa hiyo, kwa sababu sitajisikia vizuri kuchagua timu ambazo zitaiweka pagumu Brazil," alisema Pele anayepewa heshima Brazil kama mchezaji babu kubwa zaidi kuwahi kutokea nchini humo.
"Nimeshinda Makombe matano ya dunia, mawili na Santos na matatu na timu ya taifa na nimefunga mabao zaidi ya 1000, hivyo uko sahihi, nini ni babu kubwa,"alisema.



.png)
0 comments:
Post a Comment