• HABARI MPYA

  Jumatatu, Desemba 16, 2013

  BETRAM MOMBEKI ‘ALIVYOMBOA’ LOGARUSIC JANA…NA ALIVYOKOSA RAHA BENCHI, SIJUI KIATU!

  Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
  KOCHA mpya wa Simba SC, Zdravko Logarusic jana alimtoa uwanjani dakika ya 30 mshambuliaji Betram Mombeki, mara tu baada ya kukosa bao la wazi, kufuatia krosi nzuri ya Uhuru Suleiman kutoka upande wa kulia katika mchezo wa kirafiki dhidi ya KMKM ya Zanzibar, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Katika mchezo huo, ambao Simba SC ilishinda mabao 3-1, mguu wa Mombeki ulichelewa kugusa krosi ya Uhuru na ikapitiliza, huku akibaki ameshika kichwa kwa kutoamini kama amekosa bao la wazi.
  Logarusic akimpokea benchi Mombeki jana
  Wakati bado anatafakari namna alivyokosa bao hilo, akashituliwa kwamba anaitwa benchi kumpisha mshambuliaji mwingine, Tambwe Amisi.
  Logarusic alimpokea Mombeki na kumsindikiza benchi akajifunze na mshambuliaji huyo hakuwa na raha muda wote alipokuwa ameketi ‘kibandani’.
  Alionekana kama anajitetea mbele ya wenzake na akawa kama analaumu kiatu chake- yaani kwa ujumla alikuwa mtu ambaye amekoseshwa raha na kitendo hicho, ingawa kuna wakati alilazimisha tabasamu.
  Lakini kabla ya hapo alimuelekeza sana namna anavyotaka acheze

  Viongozi walishuhudia, kutoka kulia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe, Kaimu Makamu Mwenyekiti, Joseph Itang'are 'Kinesi' na Meneja Moses Basena wakishuhudia timbwili la Mombeki na Logarusic

  Lakini Logarusic kabla ya kumtoa Mombeki alimuita zaidi ya mara mbili kuzungumza naye kumuelekeza namna anavyotaka acheze, ila ni kama mshambuliaji huyo hakumfurahisha Mcroatia huyo aliyetua Simba SC kutoka Gor Mahia ya Kenya.  
  Sasa Simba SC inakwenda kambini Zanzibar leo kujiandaa na mchezo wa Nani Mtani Jembe dhidi ya mahasimu, Yanga SC Jumamosi Uwanja wa Taifa na Mombeki atakuwa na nafasi nyingine ya kutetea nafasi yake mbele ya Logarusic.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BETRAM MOMBEKI ‘ALIVYOMBOA’ LOGARUSIC JANA…NA ALIVYOKOSA RAHA BENCHI, SIJUI KIATU! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top