• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 26, 2013

  JONAS MKUDE ALIVYOITENDEA HAKI JEZI YA YANGA TOFAUTI NA FRANK DOMAYO ALIVYOIFANYIA JEZI YA SIMBA

  Frank Domayo aliivaa 'nje ndani' jezi ya Simba, kwa sababu gani sasa?
  BAADA ya mechi ya mahasimu wa jadi nchini, Simba na Yanga ya Nani Mtani Jembe Jumamosi iliyopita, wachezaji kadhaa walibadilishana jezi kuonyesha kwamba mchezo ni urafiki na si uadui.
  Katika mchezo huo, Simba SC ilishinda mabao 3-1, baadhi ya wachezaji walivalia jezi za wapinzani bila woga, lakini wengine walivaa ‘kiwoga woga’.
  Malinzi akimvalisha Medali Mkude kulia akiwa amevalia jezi ya Yanga SC
  Mkude aliivua jezi hiyo ya Yanga wakati anaondoka uwanjani

  Miongoni mwa waliovaa jezi za wapinzani kiwoga woga ni kiungo wa Yanga, Frank Domayo ambaye aliigeuza jezi hiyo ‘nje ndani’. Hii ilimaanisha nini, yeye Yanga sana, alikerwa na kipigo hadi akachukia jezi ya wapinzani, au alihofia mashabiki tu.
  Uvaaji wa jezi ya wapinzani wa Domayo ulikuwa tofauti sana na kiungo mwenzake, Jonas Mkude wa Simba SC ambaye aliivaa bila woga jezi ya Yanga SC na kwa kujiamini.
  Mkude alikwenda na jezi hiyo ya Yanga SC kuchukulia hadi Medali yake ya Dhahabu kwa mgeni rasmi, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya ushindi na akapiga nayo picha katika sherehe za kukabidhiwa Kombe.
  Baada ya hapo, aliivua akaenda kupanda basi na bila shaka amekwenda kuiweka nyumbani kwake kama kumbukumbu.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: JONAS MKUDE ALIVYOITENDEA HAKI JEZI YA YANGA TOFAUTI NA FRANK DOMAYO ALIVYOIFANYIA JEZI YA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top