• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 21, 2013

  SIMBA NA YANGA MTANI JEMBE ‘LIVE’ STAR TV

  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
  MCHEZO wa Nani Mtani Jembe baina ya mahasimu wa jadi nchini, Simba na Yanga unaochezwa leo jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, utaonyeshwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha Star.
  Mgeni rasmi katika mchezo huo atakuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe na utaanza saa 10:00 jioni.
  Nani Mtani Jembe unaandaliwa na wadhamini wa klabu hizo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager, ambao ni wadhamini wa timu hizo.
  Viungo, Amri Kiemba wa Simba kulia na Athumani Iddi wa Yanga kushoto wakimenyana katika mechi ya msimu uliopita.

  Mchezo huo, utakaochezeshwa na refa Ramadhan Ibada ‘Kibo’ kutoka Zanzibar, atakayesaidiwa na Ferdinand Chacha wa Bukoba na Simon Charles kutoka Dodoma, iwapo dakika 90 zitaisha kwa sare, sheria ya mikwaju ya penalti itatumika kuamua mshindi.
  Wachezaji wanaoruhusiwa kucheza mechi ya leo ni wale waliosajiliwa ama kikosi cha kwanza au timu ya vijana pamoja na wapya ambao wameombewa usajili katika dirisha dogo.
  Mara ya mwisho zilipokutana timu hizo Mei mwaka huu katika mchezo wa Ligi Kuu, Simba SC ilitoka nyuma kwa mabao 3-0 na kupata sare ya 3-3 Uwanja wa Taifa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA NA YANGA MTANI JEMBE ‘LIVE’ STAR TV Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top