• HABARI MPYA

  Jumatano, Desemba 18, 2013

  STRAIKA MPYA AZAM AONYESHA NI MOTO WA KUOTEA MBALI...MAANDALIZI YA KWENDA KUBEBA TENA MWALI WA MAPINDUZI YASHIKA KASI CHAMAZI

  Nahodha wa Azam FC, John Bocco 'Adebayor' akifanya mazoezi na wenzake leo asubuhi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Azam inajiandaa kwenda kutetea Kombe la Mapinduzi, michuano inayoanza Januari 1, mwakani visiwani Zanzibar.
  Mshambuliaji tegemeo kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche akinywa maji ya Uhai baada ya mazoezi 
  Mshambuliaji mpya kutoka klabu ya Stella Abidjan ya Ivory Coast, Ismael Muamad Kone (katikati) akikokota mpira mazoezini leo. Kone ameonyesha ni mchezaji mzuri na wapenzi wa Azam watarajie kuona vitu vyake kuanzia Januari katika Kombe la Mapinduzi.
  Kone akinyoosha viungo
  Kiungo Jabir Aziz Stima akinyoosha viungo

  Kocha wa akademi, Vivik Nagul ndiye aliongoza mazoezi leo akishirikiana na kocha Msaidizi, Kali Ongala wakati kocha Mkuu, Joseph Marius Omog raia wa Cameroon atawasili Ijumaa
  Gaudence Mwaikimba akikokota mpira

  Mganda Brian Umony bado yupo Chamazi

  Kipa Mwadini Ally kushoto akidaka na kulia ni kocha wa makipa Iddi Abubakar Mwinchumu

  Beki tegemeo, Aggrey Morris akichezea mpira

  Kulia beki David Mwantika

  Kone ni hatari bosi; Meneja wa Azam akizungumza na simu wakati mazoezi yakiendelea

  Wachezaji wa kikosi cha kwanza walichanganyika na wachezaji wa akademi

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: STRAIKA MPYA AZAM AONYESHA NI MOTO WA KUOTEA MBALI...MAANDALIZI YA KWENDA KUBEBA TENA MWALI WA MAPINDUZI YASHIKA KASI CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top