• HABARI MPYA

    Tuesday, December 24, 2013

    MWESIGWA KATIBU MPYA TFF, MTAWALA NAYE AULA, WAMBURA AREJEA KWENYE ‘KIOTA CHAKE’

    Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemuajiri Katibu wa zamani wa klabu ya Yanga SC, Celestine Mwesigwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa shirishiko hilo.
    Taarifa ya Rais wa TFF, Jamal Malinzi imesema kwamba, Mwesigwa amekidhi sifa za nafasi hiyo, akiwa na kiwango cha elimu ya Shahaha ya Uhusiano wa Kimataifa na Stashahada ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 
    Aidha, TFF pia imemuajiri katibu wa Simba SC, Wakili Evodius Mtawala kuwa Mkurugenzi wa Vyama na Masuala ya Kisheria ya TFF- ambaye ana Shahada ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pia na Shahada ya Uzamili ya uongozi wa Biashara ya Chuo Kikuu cha ESAMI.
    Jamal Malinzi amemuajiri Mwesigwa kuwa Katibu mpya Yanga SC anarithi nafasi ya Angetile Osiah

    Malinzi amesema, Iddi Mshangama atakaimu ya nafasi ya Mkurugenzi wa Mashindano ya TFF, iliyokuwa inashikiliwa na Saad Kawemba, wakati Danny Msangi atakaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Fedha na Utawala TFF na Boniphace Wambura Mgoyo ataendelea kuwa Ofisa Habari wa shirikisho.  
    Malinzi aliyesema ajira zote zitaanza rasmi Januari 1 mwakani, pia ameteua Kamati tatu, ya Uchaguzi, Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF nay a Soka ya Ufukweni.
    Kamati ya Uchaguzi itakuwa chini ya Mwenyekiti, Wakili Melchesedek Lutema, Makamu wake Wakili Walter Chipeta na Wajumbe Hamidu Mahmoud Omar, Jeremiah John Wambura na Hassan Daalal.
    Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF itakuwa chini ya Mwenyekiti Wakili Julius Lugaziya, Makamu wake Wakili Mwita Mwaisaka na Wajumbe Juma Abeid Khamis, Rashid Dilunga na Masoud Issangu, wakati Kamati ya Soka ya Ufukweni itakuwa chini ya Mwenyekiti Ahmed Mgoyi na Wajumbe Deo Lucas, Juma Mgunda, Boniphace Pawasa, Joseph Kanakamfumu na John Mwansasu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWESIGWA KATIBU MPYA TFF, MTAWALA NAYE AULA, WAMBURA AREJEA KWENYE ‘KIOTA CHAKE’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top