• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 21, 2013

  LIVERPOOL KAMA SIMBA SC, YAUA 3-1 SUAREZ APIGA MBILI KAMA TAMBWE

  MSHAMBULIAJI Luis Suarez ameendeleza makali yake baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa Liverpool wa 3-1 dhidi ya Cardiff jioni hii Uwanja wa Anfield.
  Nyota huyo wa Uruguay alifunga mabao yake katika dakika za 25 na 45, wakati bao lingine la Liverpool lilifungwa na Raheem Sterling dakika ya 42 wakati bao la kufutia machozi la wapinzani wao lilifungwa na Jordon Mutch.
  Ushindi kama huo imepata Simba SC nchini Tanzania leo wa mabao 3-1 dhidi ya mahasimu wao, Yanga SC na Mrundi Amisi Tambwe akifunga mabao mawili moja Awadh Juma.
  Babu kubwa: Mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez akishangilia baada ya kufunga bao la pili dhidi ya Cardiff Uwanja wa Anfield leo
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIVERPOOL KAMA SIMBA SC, YAUA 3-1 SUAREZ APIGA MBILI KAMA TAMBWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top