• HABARI MPYA

    Tuesday, December 10, 2013

    MECHI INACHEZWA NYAYO, DILUNGA AZIBA PENGO LA SURE BOY...SUDAN YAITOA ZAMBIA

    Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
    MVUA imepungua na yamebaki manyunyu kwa mbali, wakati tayari vikosi vya timu zote mbili Tanzania Bara na Kenya, vinapasha misuli moto ndani ya Uwanja wa Nyayo tayari kwa mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge ambao sasa utaanza  Saa 1:00 kufuatia kuchelewa kumalizika kwa mechi kati ya Sudan na Zambia.
    Marefa wanapasha Nyayo

    Sudan imeitoa Zambia kwa ushindi wa mabao 2-1 ndani ya dakika 120, mabao yake yakifungwa na Miaaz Abdelrahman dakika ya 117 na Salah Ibrahim dakika ya 120, wakati la wapinzani wao limefungwa na Ronald Kampamba dakika ya 113 Uwanja wa County ya Mombasa, zamani Manispaa.
    Awali, mchezo kati ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ na Kenya ‘Harambee Stars’ ilikuwa uchezwe Uwanja wa Kenyatta, Machakos Saa 7:00 mchana, lakini ukapelekwa Nyayo na kusogezwa mbele kutokana mvua kuharibu hali ya Uwanja.
    Kocha Kim Poulsen amemuanzisha kiungo Hassan Dilunga kuziba pengo la Salum Abubakar ‘Sure Boy’ anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu na kulia ameendelea kumpanga Michael Pius Aidan badala ya Himid Mao ambaye anaanzia benchi.  
    Kenya wanapasha


    Wanaoanzia benchi Stars wanapasha

    Wanaoanza Stars wanapasha

    Kikosi cha Stars kinachotarajiwa kuanza leo ni; Ivo Mapunda, Michael Pius, Erasto Nyoni, Said Morad, Kevin Yondan, Frank Domayo, Mrisho Ngassa, Hassan Dilunga, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta na Amri Kiemba.
    Kenya; Duncan Ochieng, Allan Wanga, James Situma, Aboud Omar, Joackins Atudo, Peter Opiyo, Francis Kahata, Anthony Akumu, Clifton Miheso, David Ochieng Owino na Edwin Lavatsa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MECHI INACHEZWA NYAYO, DILUNGA AZIBA PENGO LA SURE BOY...SUDAN YAITOA ZAMBIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top