• HABARI MPYA

  Jumanne, Desemba 31, 2013

  MESSI AWEKWA ‘KITI MOTO’ SIMBA, KISA? UTOVU WA NIDHAMU

  Na Mahmoud Zubeiry, Azam Marine
  KIUNGO nyota wa Simba SC, Ramadhani Yahay Singano ‘Messi’ leo asubuhi aliwekwa kikao cha dharula na viongozi wa klabu yake, kwa kuonyesha kitendo cha utovu wa nidhamu wakati wa safari ya timu hiyo visiwani Zanziabr kwenye Kombe la Mapinduzi.
  Wachezaji wa Simba SC wakiwa bandari ndogo ya Azam Marine, Dar es Salaam asubuhi tayari kwa safari ya Zanzibar, Messi alifika akiwa hana jezi ambayo wachezaji waliagizwa wavae wakati wa safari.
  Umeanza kuvimba kichwa? Viongozi wa Simba SC, kutoka kulia Moses Basena, Said Pamba na Ibrahim Masoud wakizungumza na Messi kushoto leo asubuhi

  Kitendo hicho kiliwaudhi Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba SC waliokuwa wanaongoza msafara, Ibrahim Masoud ‘Maestro’ na Said Pamba ambao walilazimika kumuita pembeni mchezaji huyo kumuhoji.
  Baada ya utetezi wake, ilibidi na Meneja wa timu, Mganda Moses Basena aitwe kutoa ushahidi. Hata hivyo, Basena alionekana kutokubaliana na maelezo ya Messi, lakini viongozi wakaachana naye aendelee na safari.
  Messi amekuwa kipenzi cha wana Simba SC tangu Desemba 21, mwaka huu acheze kwa kiwango cha juu katika mchezo dhidi ya mahasimu, Yanga wa Nani Mtani Jembe na kusaidia ushindi wa mabao 3-1.
  Bila nidhamu, mpira utakushinda; Messi akiwasikiliza viongozi wake
  Hii siyo sare yetu ya safari; Basena akizungumza huku ameshika fulana ya Messi...Halafu tazama Maestro alivyokasirika...Pamba naye...

  Inaonekana kama sifa alizozipata baada ya mchezo huo, zinaanza kumfanya ajione yuko tofauti na wachezaji na wenzake, jambo ambalo viongozi wa klabu hiyo wanaonekana mapema kuanza kupambana nalo.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MESSI AWEKWA ‘KITI MOTO’ SIMBA, KISA? UTOVU WA NIDHAMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top