• HABARI MPYA

  Jumanne, Desemba 31, 2013

  USAJILI DIRISHA DOGO MAMBO MAGUMU MAN UNITED, MTENDAJI MKUU AGOMA KUMPA MOYES FEDHA ZA KUNUNUA WACHEZAJI WAPYA

  KLABU ya Manchester United inahofia jitihada zake za beki mpya wa kushoto katika usajili wa dirisha dogo Januari hauwezi kuvunja matunda, kwa Everton na Southampton kutokuwa na mpango wa kuwaachia wachezaji wake Leighton Baines na Luke Shaw.
  Kocha wa United, David Moyes alijaribu bila mafanikio kutaka kumsaini Baines kutoka klabu yake ya zamani mapema msimu huu, baada ya Patrice Evra kusema anahitaji ushindani wa maana wa namba katika nafasi yake.
  Lakini juhudi za United zimezimwa na Mwenyekiti wa Everton, Bill Kenwright na pamoja na hayo Moyes ameambiwa na Mtendaji Mkuu wa klabu yake, Ed Woodward kwamba hana fedha za kutoa kwa ajili ya usajili wa mwezi ujao.
  Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England wanahofia watakutana na mazingira yale yale kutoka klabu ya Merseyside, pamoja na Southampton juu ya Shaw wanayemtaka.
  Anatakiwa; Man United imeendelea kumuwania Leighton Baines
  Teen sensation: Luke Shaw, 18, is destined to be picked up by a bigger club than Southampton but not yet
  Watchful: David Moyes is keen to bolster his defence in the transfer window
  Anaowatolea macho: David Moyes anamtaka Baines na beki wa Southampton, Luke Shaw, lakini kuna hatari akawakosa

  Shaw, mwenye umri wa miaka 18, pia yupo kwenye rada za Chelsea, lakini Southampton imeweka wazi kwamba haimuuzi mchezaji huyo. 
  United inahaha kusaka beki wa kushoto kutokana pia na Mholanzi, Alexander Buttner kushindwa kufanya vizuri tangu asajiliwe na Sir Alex Ferguson mwaka 2012. 
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, binafsi anatakiwa na Tottenham katika usajili huu wa Januari, ameanza katika mchezo mmoja tu wa Ligi Kuu msimu huu, maana yake kwamba Evra, akiwa na umri wa miaka 32, amebeba majukumu makubwa ya timu katika nafasi hiyo. 
  Tayari msimu huu, beki huyo wa Ufaransa amecheza mechi 29 za klabu yake na hi yake katika mashindano yote.
  Heavy workload: With no back-up up to scratch, Patrice Evra's played most games at left back this season
  Majukumu mazito: Akiwa hana msaidizi wa maana, Patrice Evra amecheza mechi nyingi beki ya kushoto msimu huu

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: USAJILI DIRISHA DOGO MAMBO MAGUMU MAN UNITED, MTENDAJI MKUU AGOMA KUMPA MOYES FEDHA ZA KUNUNUA WACHEZAJI WAPYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top